KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumatano, 16 Aprili 2014
HUU NI UKATIRI ULIOPITILIZA.
Haimuingii akilini mtu yoyote aliesoma na asiekwenda shule kabisa kuona baadhi ya watanzania (na mimi nashawishika kusema kuwa mtu anaekuwa na ujasiri wa kutenda kitendo hiki sio mtanzania halisi)wanafanya vitendo vya kusikitisha kama hivi.
Hakuna mtu asiejua umuhimu wa twiga katika nchi hii ukiachilia mbali kuwa ni nembo ya taifa,jambo ambalo linatosha kuwa waangalifu sana katika kuwalinda wanyama hawa kwani kuwa nembo maana yake ni kuwa wanyama hawa wanapopotea na Tanzania inapotea katika utambulisho wake kimataifa.
Nimesema maneno haya kwa uchungu na hasira baada ya mtu mmoja asie kuwa na hata chembe ya huruma kumgonga na kumuua twiga katika hifadhi ya wanyama ya Katavi tukio ambalo linasikitisha sana.
Twiga huyo ambae anaonekana kuwa alikuwa anavuka barabara aligongwa na mtu huyo ambae hajafahamika ni nani na gari yake ni ya aina gani.Jambo hili ni la makusudi kwasababu unapofika katika hifadhi lazima ujue kuwa wanyama huwa wanakatiza kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine.Pia hakuna asiemfahamu twiga ambae ni mnyama mpole na mwenye mwendo wa taratibu sana kwa hiyo dereva yoyote anaejua kuwa mahari anapopita pana twiga angepunguza mwendo kwa tahadhari.Matukio haya ni mabaya sana na yanapaswa kulaaniwa kwa nguvu zote.
Picha hizi zinamuonesha twiga akiwa amekufa baada ya kugongwa na gari na mtu asiefahamika akitazamwa na maafisa wa wanyama pori TANAPA.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni