Kurasa

Jumatano, 2 Aprili 2014

HISTORIA YA TAJIRI NAMBA MOJA AFRICA ALIKO DANGOTE #THE HISTORY OF THE RICHEST PERSON IN AFRICA ALIKO DANGOTE#


Aliko Dangote alizaliwa Nigeria mwaka 1957,april,10.Historia ya utajiri katika familia yake ilianzia kwa babu yake ambae alikuwa na mashamba makubwa ya peanut ambazo zilikuwa zikisafirishwa kwenda ulaya na kufanikiwa kupata utajiri mkubwa.



Moyo wa kijasiliamali ulikuwa ndani ya damu ya Dangote kwani akiwa shule alianza kufanya biashara ya mishumaa.Baada ya kupata shahada yake katika chuo cha Al- azhar huko Misri ambayo ilikuwa ni shahada ya biashara,alianzisha kampuni yake ya kwanza ambayo iliitwa DANGOTE GROUP ambayo ilihusika na biashara ya Cement.Kwa wakati huo tayari familia yake ilikuwa na uhusiano mzuri na serikali na kwa hivyo ilikuwa rahisi kwake kupata leseni bila matatizo.Swala la kupata leseni Nigeria ni gumu sana.

Baada ya hapo Dangote alifanya biashara katika nchi mbalimbali kama Brazil,Amerika ya Kusini ambako alipata mafanikio makubwa sana ya kibiashara.Aliweza kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwemo nyumba aliyokuwa ameijenga huko Atlanta.Hata hivyo aliamua kurudi Nigeria na kuirudisha biashara yake Nigeria ili kukuza uchumi wa nchi hiyo.

Aliporudi Nigeria miaka ya 90 Dangote alikisaidia chama cha PEOPLES DEMOCRATIC PARTY na kiliposhinda alifanikiwa kuishawishi serikali kumruhusu kujenga moja kati ya viwanda vikubwa kabisa vya cement nchini Nigeria.Kwa sasa Dangote ana wafanyakazi zaidi ya elfu ishirini na tano(25000) na anafanya biashara katika nchi kumi na nne Afrika nzima.

Mafanikio ya Dangote ni mengi kiasi kwamba unaweza kujaza vitabu kadhaa lakini kwa kifupi anafanya biashara nyingine kama chumvi,unga wa ngano,cocoa,sukari nk.Ana nguvu kiasi kwamba ni rafiki mkubwa na tajiri namba moja duniani bwana Bill gate na anapoongea Gate humsikiliza.

Hongera mr Dangote na hongera kwa baadhi ya watanzania kama Rostam Aziz,Mengi,MO pamoja na Bakhresa kwa kuingia katika orodha ya matajiri Afrika na duniani kwa ujumla na kutuonesha njia.Pia hii inatukumbusha kuwa nchi zetu za kiafrika sio maskini bali sisi ndio wavivu wa kufikiri na kuzifuata fulsa.

BILL GATE AKIMSIKILIZA ALIKO DANGOTE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni