Kurasa

Jumamosi, 19 Aprili 2014

HALI TETE!

Huku makubaliano yalioafikiwa siku ya alhamisi ya kupunguza hali ya wasiwasi nchini Ukraine yakikabiliwa na changamoto,waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewapigia simu maafisa wakuu katika serikali za Ukrain na Urusi.
Afisa mmoja wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani amesema kuwa bwana kerrry ameiagiza serikali ya Urusi kuafikia mkataba huo kikamilifu na mara moja.
Pia ameipongeza serikali ya Ukraine kwa hatua ilizochukua kuafikia mkataba huo.
Siku ya ijumaa wanaharakati wanaounga mkono Urusi walikataa kuondoka katika majengo wanayodhibiti mashariki mwa Ukraine,wakisisitiza kuwa uongozi mpya wa Ukraine ni sharti ujiuzulu kwanza.
Serikali ya mpito nchini Ukraine imetoa wito wa umoja wa kitaifa, ikiahidi kugatuwa mamlaka mbali na kuwahakikishia wakaazi wa eneo hilo la mashariki kwamba lugha ya kirusi itaendelea kuzungumzwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni