Kurasa

Jumanne, 29 Aprili 2014

GUADIOLA AUHARIBU MPIRA WA BAYANI,WAUONA MOTO KWA MADRID.

Tuesday, April 29, 2014
UEFA CHAMPIONS LEAGUE..LIVE MATCH: BAYERN MUNICH 0 vs REAL MADRID 4, (Agg 0-5) SERGIO RAMOS NA RONALDO WAWAZIMA BAYERN ALLIANZ ARENA!!
Real Madrid Usiku huu wameitawanya timu ya Bayern Munich bao 4-0 (Agg.5-0) na kwa matokeo hayo Real wanasonga mbele wakisubiri mshindi wa kesho jumatano kati ya Chelsea na Atletico Madrid. Bao za Real zimefungwa kipindi cha kwanza na cha pili. Dakika ya 16 kipindi cha kwanza Sergio Ramos anaifungia bao tamu la kichwa Real Madrid baada ya kupokea mpira uliopigwa na Luka Modric. Dakika ya 20 tena Sergio Ramos anafunga bao la pili na kufanya 2-0 dhidi ya Bayern na kwa kichwa tena baada ya kukwea kichwa hicho mpira uliopigwa na Pepe. (Agg: ni 0-3).
Dakika ya 34 C. Ronaldo anaifungia bao la tatu baada ya kupokea pasi kutoka kwa Bale!! Bao hilo la Ronaldo linaongeza Agg. kuwa 4-0. Dakika za lala salama Ronaldo anafunga bao la mwisho la nne na kufanya 4-0 huku Agg. Ikiwa ni 5-0 dhidi ya Bayern Munich
VIKOSI:
Bayern Munich:Neuer; Lahm, Dante, Boateng, Alaba; Schweinsteiger, Kroos; Ribery, Muller, Robben; Mandzukic
Subs:Raeder, van Buyten, Martínez, Rafinha, Pizarro, Gotze, Hojbjerg
Real Madrid:Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos, Coentrao; Alonso, Modric; Di Maria, Ronaldo, Bale; Benzema
Subs:Diego Lopez, Varane, Marcelo, Casemiro, Morata, Isco, Illarra

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni