Kurasa

Jumatano, 16 Aprili 2014

DIAMOND ATOBOA SIRI KUWA ANA MTOTO ALIPOKUWA ANAHOJIWA NA MTANDAO WA NIGERIA

Nani aliyekuwa anafahamu kuwa Diamond Platnumz ni baba? Well, hatujawahi kumsikia popote akisema kuwa ana mtoto lakini staa huyo wa ‘My Number One’ alikuwa mkarimu wa kutosha kuweza kuelezea ‘furaha ya kuwa mzazi’ kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao maarufu wa Nigeria uitwao Lobatan Africa baada ya kwenda huko wiki kadhaa zilizopita alikoshirikishwa pia na mastaa wa huko wakiwemo Waje na Dr Sid.

Kwenye mahojiano hayo, mtandao huo ulimuuliza: What have you learnt about fatherhood, now that you’re a father (umejifunza nini kuhusu ubaba kwakuwa sasa wewe ni baba)

Diamond alijibu: Fatherhood is a great experience, very humbling. You learn a lot about your children and the kids and the kinds of things they love. For example, my baby loves this cartoon that has a catchy song, I think Ben10. Hahaha!! (Kuwa baba ni kitu kikubwa, kinavutia sana. Unajifunza mengi kuhusu watoto wako na vitu wanavyopenda. Kwa mfano ‘mwanangu’ anapenda katuni hii yenye wimbo unaogusa, nadhani Ben 10!

Kumbe Diamond ana mtoto tena mkubwa anayeweza kuangalia na kuelewa katuni? Swali ni kwanini hajawahi kusikika akisema ana mtoto? Hata hivyo September mwaka jana, moja ya magazeti ya udaku ya kampuni ya Global Publisher, yaliandika habari ya kuibuka kwa msichana aitwaye Sasha Juma aliyedai kuwa amezaa na Diamond.

Sasha akiwa na mtoto anayedai ni wa Diamond
Msichana huyo alidai kuwa likutana na Diamond Mlimani City jijini Dar es Salaam na akampenda kwakuwa anafanana na Wema Sepetu (kipindi hicho walikuwa wameachana. Gazeti hili lilisema wawili hao hawakuchukua muda na wakaanza uhusiano uliowafanya wakutane kimwili na kupelekea msichana huyo kushika ujauzito.

Lilidai asha alimpa taarifa staa huyo ambaye alimuomba asitoe mimba kwakuwa atamsomesha msichana huyo aliyefukuzwa shuleni na pia kuahidi kumlea mtoto huyo.

“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” gazeti hilo lilimnukuu Sasha.

Lilisema lilipomtafuta Diamond kwa simu ambaye kwa sasa yupo nchini Kenya, alijibu: Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni