Kurasa

Jumapili, 27 Aprili 2014

ANGALIA JINSI BABA ALIVYOMUUA MTOTO WAKE KWA KUMTWANGA NGUMI,KATIKA TAARIFA HII YA POLISI MBEYA.

Sunday, April 27, 2014
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 27.04.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAVANESA PATRICK NJOJO(03)MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYEPATRICK NJOJO(23)MKAZI WA ISISI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE26.04.2014MAJIRA YA SAA23:45USIKUHUKO KATIKA KIJIJI CHAISISI,KATA NA TARAFA YARUJEWA,WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA4 – 5ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LAFESTO MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILISM 9124AINA YAFAWLILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVARAMADHANI MWALYOYO (30)MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE26.04.2014MAJIRA YA SAA14:45 MCHANAHUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGIANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
Signed by:
[A HMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni