Kurasa

Jumatatu, 3 Februari 2014

MWIKO WA MBEYA CITY WAVUNJWA NA YANGA

Ule mwiko wa timu iliyoko ligi kuu ya Tanzania Bara Mbeya city umevunjwa wa kutokufungwa toka kuanza kwa ligi kuu Tanzania Bara umevunjwa jana baada ya kukubali kichapo cha bao moja kwa bila kutoka kwa wapinzani wao timu ya Yanga uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Bao hilo la pekee la Yanga lilifungwa na mshambuliaji mahili Mrisho khalfan Ngasa katika dakika za mwanzoni za kipindi cha kwanza na bao hilo kudumu katika muda wote ambao mchezo huo ulifanyika.

Wakizungumza kwa furaha na muandishi wa habari hii mashabiki wa timi ya Yanga waliokuwa wamefurika uwanjani hapo walijigamba kuwa swala la Mbeya city kufungwa lilikuwa la lazima ili kujihakikishia nafasi nzuri katika kinyanganyiro hiki cha ligi kuu Tanzania Bara.

Kwa upande wao mashabiki wa Mbeya City walisema kuwa matokeo yaliyopatikana ni matokeo ya mpira wa miguu na kama inavyofahamika katika mchezo huo kuna kufungwa kutoa droo au kushinda kwa hiyo wao hawakati tamaa na wanajipanga kwa mchezo mwingine unaofuata kwakuwa matumaini yao ni kunyakua ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.

ZIFUATAZO NI PICHA ZINAZOONESHA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MTANANGE HUO.

PICHA ZOTE KWA HISAN YA OTHMAN

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni