KARIBU SANA MUKEBEZI BLOG #SAUTI YA WATU#. BLOG YA HABARI ZISIZO ZA KAWAIDA NA UJASIRIAMALI INAYOONGOZA TANZANIA.
Kurasa
▼
Jumanne, 18 Machi 2014
WALICHOKIFANYA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA NI UTOVU WA NIDHAMU.
Siku ya jumatatu ya tarehe 17 march 2014 jaji mstaafu mzee Joseph Sinde Walioba alitaka kuwasilisha rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania tayari kwa kujadiliwa hoja moja baada ya nyingine lakini kwa bahati mbaya alishindwa kutokana na wajumbe wa bunge maalum kufanya fujo kwa kugonga meza na hivyo kutokuwepo na kusikilizana bungeni hapo.
Sina haja ya kurudia kusimulia sababu zilizotolewa na wabunge hao kutetea kitendo chao hicho cha kuzuia Mzee Walioba asiwasilishe rasimu hiyo kwani ni hoja ambazo hata mtoto mdogo atakwambia kuwa hazina mashiko.
Nasema hoja hizo hazina mashiko kwasababu lengo kuu la wajumbe hao kuwepo Dodoma sio hotuba ya Rais au chochote wanachokisema, isipokuwa swala lililowapeleka hapo ni Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo Rasimu yake ndio mzee Warioba alitaka kuiwasilisha ili ijadiliwe.
Kutokana na matukio mbalimbali yanayoendeelea kujitokeza bungeni ambayo mengine hata watoto wadogo wanashangaa kuona kuwa hata watu wazima wanafanya matendo hayo,wananchi wanafika mbali na kudiriki kusema kuwa hizo ni mbinu za kutaka siku ziongezeke na wabunge hao waendelee kuwepo bungeni hapo na kuendelea kula posho zinazotokana na kodi ya wananchi walala hoi wa nchi hii.
Ni dhahiri shahiri kuwa wabunge hawa wanajua wanachokifanya bungeni,ikiwa na maana kuwa wanajua lengo la kufanya vitendo hivyo,na kama watasema hawajui wanachkifanya basi hoja hiyo itakuwa inakwenda mbali zaidi, kwa sababu kuwaweka watu ambao hawajui wanachokifanya halafu tunategemea watoke bungeni pale wakiwa na katiba ambayo itatuongoza wananchi zaidi ya milioni arobaini tena kwa zaidi ya miaka hamsini litakuwa ni jambo la kushangaza kidogo.
Wabunge hawa wanapaswa kufahamu kuwa hichi wanachokifanya sasa kitawaathiri na wao wenyewe pamoja na watoto wao vizazi kwa vizazi vijavyo kwa hiyo bado wana muda wa kujirekebisha na kuongeza umakini katika mambo ya msingi kama hayo.